Diamond Platinumz

SHHH! Diamond Platinumz Azimwa Hewani Ghafla Bin Vuu

Reading Time: < 1 minute

Diamond Platinumz Matatani

Kwa siku saba Diamond Platinumz hawezi sikika hewani. Hii ni baada ya brand yake moja kukera serikali ya Rais John Pombe Magufuli. Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifunga kituo cha Wasafi FM inayomilikiwa na msanii huyo superstar wa bongo flava.

Kuanzia September,12 2020 wasafi FM haiwezi ruhusiwa kupeperusha habari zake na kuendesha vipindi vyake nchini Tanzania.Mkurungezi mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba alitoa agizo hilo ijumaa.

Wasafi FM Yachafua Mawimbi ya Hewa 

Wasafi FM kupitia show zake pili ‘The Switch’ na ‘Mashamsham’ inakisiwa kutumia lugha isiyo ya staha hewani mnamo tarehe Augosti 1 saa mbili usiku na Agosti 4 saa 5pm kinyume na kanuni na taratibu za mawasaliano ya kielektroniki namba 11.

Omary Rajabu Tambwe AKA lilommy, Ammy Gal na Ray Mshana ndo mapresenter kwenye show ya The Switch.Watatu hao mabigwa walitambulizwa na Diamond march kuliendesha show hiyo ambayo inahoji wanamuziki na kuangazia mitindo na nyimbo mpya.

“Hawa ndio mafundi wa burudani Afrika Mashariki ambao kuanzia leo watakuwa wanakusogezea Info zote  za kijana, interviews kali na ngoma zote kali kupitia the Switch,” Wsafi TV ilitangaza.

Pamoja na kuzimwa hewani Wasafi FM iliamrishwa kuomba msamaha kwa tume hiyo na kwa watanzania wote. 

1586

Leave a Reply

Pin It on Pinterest

error: Alert: Content is protected !!