Sababu 8 Zinazofanya Wanawake Watanzania Kupendwa sana na Wanaume

Reading Time: 4 minutes

Utamu wa Wanawake Watanzania

Je ushawahijiuliza mbona wanaume wengi haswa Afrika ya Mashariki huwapendelea sana wanawake watanzania? Uchunguzi unabaini ya kwamba, saba kati ya wanaume kumi nchini Kenya, wanatamani kuwa na uhusiano na banati mtanzania.Hili limefanya tuwe na kiu ya kutaka kujua kwa undani sababu ambazo zinafanya wanaume wengi wawe na tamaa kubwa sana ya kuchumbiana na vipusa kutoka nchi ya Tanzania.

Sababu 8 Zinazofanya Wanawake Watanzania Kupendwa na Wanaume. (pinterest)

Kwa hivyo kina dada wa kutoka pande ile nyingine, niwie radhi, sijawadhalalisha ila tu ukweli lazima usemwe. Huenda nisemalo hapa kuhusu malkia watanzania, madume wa Tanzania pia watasema kuwa husu nyinyi. Maana wahenga walisema, ganda la mua la jana chungu kaona litamu. Ni ukweli, kunao kutoka nchi nyingine walio na tamaa ya kuchumbia vidosho wa humu nchini. Kila mja na mvuto wake.

Je wewe binafsi, ushawahi kuwa na matamanio ya kumchumbia kidege mtanzania? Kama ndio basi,ni  dhahiri kwamba siko peke yangu. Nyuma ya hili pazia la ndoto, kuna mvuto fulani.

Ukweli wa mambo ni kwamba, mbali na urembo halisia wa hawa vichuna kutoka nchi ya Mwalimu Nyerere, kuna mambo fichu ambayo wakati mwingine hayasemwi vivi hivi pasipo kuzingatia  mazingira.

# 1 Wanenguzi hodari wa viuno

Sababu 8 Zinazofanya Wanawake Watanzania Kupendwa na Wanaume. (Twitter)

Kwa wale ambao tayari wamewahi zari ya kuchuna ngozi kidosho kutoka Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania,wanaafiki kuwa, hawa warembo ni wanenguzi hodari wa viuno. Kunengua kiuno kuna umuhimu gani wakati wa kufanya mapenzi? Wataalam wa mapenzi wanasema kwamba tendo la kutikisa kiuno na viungo vingine mwilini unasaidia kusambaza hisia za mahanjamu kila sehemu mwilini kutoka utosini hadi kwa kidole cha mguu.

Also Read: WTF: 5 fucks about Vera Sidika

Ndio maana tunaimbiwa na Zuchu, “sugar sukari”, ina maana, pindi mwili unapotikisika, utamu unazidi kutambaa katika sehemu zote husika. Mbona nawe usimpe jibu lake Nandi, “…raha tupu kupendana na wewe.”?

Tendo la ngono, sio kama kumega kiporo cha sima, bali ni kama kuchambua mpunga,lazima utikise uteo.

# 2. Ustaarabu kila pahali na vilivile kila mida

Ijapo kuna watu ambao huseme kwamba ustaarabu mwingi unaudhi, hakuna mwanaume asiyeyeyushwa na binti mwenye upole na unyenyekevu. Hebu tafakari, utajihisije ukiwa na mwanamke mstaarabu kwa kila jambo? Utaudhika? Labda uwe umepandwa na pepo mchukia ustaarabu. Upole na unyenyekevu katika machumbiano ni mfano wa dawa za kuongeza nguvu za kiume, asha kumsi matusi. Sauti nyororo ya, “samahani mpenzi wangu…”, inaamusha hisia za mapenzi. Wanaume, tuache kudanganya eti katika kuchumbiana tunabeba roho ya kijambazi au ijulikanavyo kwa king’eng’e kama“Gangster”. Hata joka lenye sumu kali hutolewa pangoni kwa maneno matamu.

# 3. Magwiji wa kutongoza

Sababu 8 Zinazofanya Wanawake Watanzania Kupendwa na Wanaume. (wikipedia)

Ujuzi na uzoefu halisia wa kurai na kutongoza wapenzi wao kwa vitendo vizuri. Hebu jiweke kwenye muktadha huu, umetoka kupiga kazi ya  kijungu meko ama hata ya kufunga tai.Jioni imefika,umechoka na umerudi nyumbani. Mlangoni unakutana na jike lako, limefunga jileso lenya maandishi ya kuvutia, “Karibu nyumbani dume, unahisi njaa naomba uniume.” Kisha unakumbatiwa, mwili wake tayari umelegea, mashumshum kwenye shavu lako,mapaja yake yanarindima. Unavuliwa koti, ama shati, unaelekezwa kwenye kiti kisha unaandaliwa maji ya kukoga mwili. Hivi mbona usitekwe mawazo na fikra?

# 4. Wavumilivu

Wanawake watanzania hasua wale wa sehemu za mashinani pia wanajua kuvumilia shida na misukosuko katika mapenzi ama ndoa. Wanathamini mapenzi kuliko pesa ama vitu vingine. Filosofia yao ni mapenzi huzidi mali.Maanake, mapenzi ni hisia, mali ni hali.Hali hubadilika, na pasipo mapenzi panakithiri ushenzi.Kwa hivyo inamaanisha kwamba huyu mwanamke anakupenda jinsi ulivyo.Mapenzi huria na halisia.

# 5. Wanajua kuliwaza

Videge watanzania vilevile, hujua kutia moyo na kuliwaza.Mambo yanapoende msegemnege,utasikia mwanadada akimweleza mchumba wake, “Mpenzi wangu, usiwe na tumbo joto, yote yatapita.La muhimu niko nawe,hutaelekea jiwe.” Hakuna kitu kizuri kwenye mapenzi kama kuwa na mchumba anayekuhakikishia upendo wake sanasana wakati wa shida.Huu ni mvuto maalum. Utajifunga kibwebwe, na kuhakikisha kuwa maazimio yako na huyu sabuni ya roho yako, yanatimika.

# 6. Umbo zuri

Sababu 8 Zinazofanya Wanawake Watanzania Kupendwa na Wanaume. (BellaNaija)

Kwa mwanaume, kabla ya hisia moyoni, lazima kuwe na tamaa machoni. Unakipata ukionacho. Kwa hivyo tamaa ya kuguza lazima iletwe na mvuto fulani.Hawa sista du kutoka Tanzania wametunukia viuno vya nyigu, ngozi nyororo,shingo za upanga na macho ya gololi. Kaka braza wanizimia sana maumbo haya.

Also Read: Popular celebrity crushes that went viral in Tanzania

# 7. Mavazi ya kuvutia

Mwanamke mtanzania hasua yule anachumbiwa ama yule anadhamiria kupata mshikaji, huwa anajitwika mavazi yenye kusisimua hisia fulani na mjadala fuatilizi. Kama ni leso, maandishi ni ya kumsifu mchumbake ama kama bado yupo uwanjani kutafuta, ya kumualika mshikaji kwenye uchumbianaji. Kwa mfano, “Huyu mume ni wangu.Yeye hunifikisha kwa mawingu.” Ama, “Nikaribishe ndani wewe mume, nimechoka kuketi nje kama paka shume.”Jike la Tanzania likikuvalia dera, bila shaka utataka kulidara.

# 8. Wanajua kuvaa chumbani 

Sababu 8 Zinazofanya Wanawake Watanzania Kupendwa na Wanaume. (mpekuzi)

Mwanamke mtanzania halisia akiwa hadharani, ni kama mtawa lakini ni hawara chumbani. Wanawake wa nchi zingine ni hawara hadharani lakini watawa chumbani. Itakuaje unaanika mapaja mbele ya halaiki, lakini ukirudi chumbani unavalia kama mwanasayansi akizuru nyota ya Mwezi?

Ningetaja mambo mengi tu, ila mda ulinikwepa.

Also Read: Wolper is a serial cheater who wanted to sleep with Diamond – Harmonize

2477

Leave a Reply

Pin It on Pinterest

fr_FRFR