Ukoloni Katika mapenzi 1

Ukoloni Katika mapenzi

Reading Time: 3 minutes

Macho sawa, maskio hamna shida, mdomo fyata!

 

Ukoloni Katika mapenzi 2

 

Je, ushawahikuwa kwenye uhusiano ambao unahisi kana kwamba huna nafasi ya kujieleza ama kwa ufupi huna uhuru  na nafasi ya kutoa maoni huria? Nimewahi ongea na watu kadhaa ambao uhusiano wao aidha wa kindoa ama wa kuchumbiana umesambaratika, na ambao wamenieleza kuwa ukosefu wa uhuru wa kujieleza ulisababisha kuvunjika kwa uhusiano.

Najua uhusiano wa kujitolea huwaunganisha watu wawili, lakini uhuru hauwezi kupotea kwa amri ya mshirika mmoja mwenye kasumba ya kikoloni.Kuwa kwenye uhusiano si kuwa korokoroni. Je wewe binafsi unawezastahili mazingira ambayo sheria ni sikiliza, angalia, tenda, na usiongee? Yaani,uhusiano wa kodoa macho-fungua-maskio-fyata ulimi. Iwe ni mwanamke ama mwanaume, bila kuzingatia uwezo wako katika jamii, mwenzako ni lazima awe na uhuru usio na kikomo wa kueleza mawazo yake.

Katika Katiba nyingi tu duniani, inasemekana tuna uhuru wa kusema na uhuru wa kujieleza. Kwa mawazo yangu, isipokuwa uhuru huo ni kamili, sio uhuru hata kidogo.Inasemekana, kuna wachumba ambo, kwa sababu wanatoka katika malezi duni, wangependelea kukaa katika uhusiano kama huo na kupata sehemu ya jina la “tajiri” kuliko kusema mawazo yao na kupoteza jina kubwa ama umaarufu fulani. Je si huo ni ukoloni mambo leo? Uhusiano kama huo si ni sawia na mnada wa watumwa? Ni nini muhimu, hela kiasi na uhuru kamali ama hela nyingi, jina kubwa bila uhuru wa kujieleza?

Hapa nchini Kenya, kukosa uhuru wa kujieleza katika uhusiano uwe wa ndoa ama kuchumbiana, kunaitwa, “Kukaliwa”. Ni sawia na mdomo wako uekwe zipu, na ufungwe, macho  yaunganishwe na darubini, ili yazidi kuona kwa  umbali na upana, na masikio yawekwe kinasa sauti.Asha kumsi matusi, kama wewe ni mwanaume mwenye hulka ya kuzima mpenziwo, heri umchumbie ama umwoe binti bubu na vile vile kama wewe ni jike lenye kasumba ya kumnyamazisha mume wako asijieleze kimawazo, heri uelekee jiwe.

Pia soma: Kwa nini Mwanamke hupiga nduru wakati wa kusakata Ngono

Ndio maana watu wameamulia uhusiano bila masharti. Na maanisha uhusiano wa funga fungua ama ingia toka. Wengi haswa kina dada wenye maumbile ya kupendeza na nyuso za kuvutia, wanapendelea mahusiano kama haya. Ili kujinafasi naye, utalipia uwepo wake na kitu chochote kingine ambacho atakutumbuiza nacho. Tizama kina dada hawa warembo, na ujivinjari nao iwapo huhitaji uhusiano wenye maongezi mengi.Pia kuna ghulamu watanashati kutoka kila sehemu barani Afrika, kama nchi ya Ivory Coast. 

Hata hivyo, huenda kuna sababu ambazo zinazofanya watu wengine wapende kuzuia uhuru wa kujieleza.Ili tusielekeze lawama bila kuzingatia sababu zinazochangia mwenendo huu, ni vizuri kuchumbua kwa mapana na marefu.

# 1. Aina ya kazi

Huenda uko kwenye uhusiano na mtu ambaye anafanya kazi ya ujasusi. Watu kama hawa huofia kufichuka kwa kazi zao ndio maana hawependi sana mazungumzo iwe ni ya kujieleza ama kupeleleza mambo fulani. Kazi nyingine ni wizi, ukiwa kwenye mahusiano na mwizi ama jambazi, kazi yako ni kunyamaza na kuponda mali aliyoiba almuradi usimwambie hupendi kazi anayoifanya.

 

Ukoloni Katika mapenzi 3

# 2. Ubinafsi

Kuna wachumba ama wanandoa ambao ni wa binafsi. Hawa watu hufikiria kwamba ni semi zao tu ndio muhimu na za wengine hazina maana. Pindi unapojaribu kujieleza, anakwambia, wacha ni kuambie, we hujui.

 

# 3. Kasumba ya jinsia

Kuna mchumba atakwambia, we ni mwanamke hufai kuongea! Ama, we ni mwanaume, unaongea kama mwanamke! Hisia aachia kina dada, eti, mwanaume ni shujaa wa vitendo wala sio maneno.

 

# 4. Madharau

Kuna wachumba walio tu na mazoea ya kuwadharu, hasua wakiwa wao ndio wenye hela na uwezo wa kusababisha kila kitu katika huo uhusiano. Kama umetoka katika familia ya umaskini, na mchumba wako katika familia bwenyenye, mara nyingi, unanyimwa sauti ya kujieleza.

Tisa yote kumi, iwapo huna shida na uhusiano ambao hurusiwi kuongea, maisha ni yako. Huenda kufyata ulimi ni muhimu sana kuliko maongezi. Lakini fikra huria ndio ratili itakayoruhusu uwazi wa mambo katika karne hizi na zijazo.

 

Ukoloni Katika mapenzi 4 1594

Leave a Reply

Pin It on Pinterest

fr_FRFR